Ilisasishwa: Septemba 2026
1. Kukubali Masharti
Kwa kusajili akaunti au kutumia Kijiji Tanzania, unakubali Vigezo na Masharti haya. Usikubali? Tafadhali usitumie huduma zetu.
2. Huduma Zetu
Tunatoa miongoni mwa huduma zifuatazo:
- Uuzaji / uwekaji wa bando la data (hasa Halotel).
- Huduma za Nakala: TIN, Nakala ya NIDA, na Leseni za Biashara (Halmashauri).
- Usaidizi wa usajili wa Lipa Namba / Merchant na Uwakala kwa mitandao mbalimbali.
- Chat na msaada kwa wateja.
Baadhi ya huduma zinategemea uthibitisho, malipo, na michakato ya nje (mfano control number ya leseni). Hatuhakikishii muda kamili wa kukamilika kwa kila ombi.
3. Akaunti yako
- Unawajibika kuweka taarifa sahihi na salama ya akaunti yako.
- Usitoe nenosiri lako au OTP kwa mtu yeyote.
- Tunaweza kuzuia au kufuta akaunti inayokiuka masharti haya au inayotumiwa kwa udanganyifu.
4. Malipo
- Bei zinaonyeshwa kwenye app kabla ya kuthibitisha.
- Malipo hufanywa kupitia ClickPesa (USSD Push) au njia nyingine tulizotaja.
- Baada ya malipo kuthibitishwa, ombi linaingia kwenye mchakato wa kushughulikiwa.
- Kwa leseni: ada ya huduma inalipwa kwenye app; control number na ada rasmi ya Halmashauri ni jambo tofauti.
5. Majukumu ya Mtumiaji
- Toa taarifa sahihi na kamili (hasa NIDA, majina, eneo).
- Usitumie huduma kwa madhumuni haramu au udanganyifu.
- Usiwasilishe hati bandia au taarifa za mtu mwingine bila ruhusa.
- Heshimu maamuzi ya mamlaka zinazohusika (mfano Halmashauri, TRA, NIDA).
6. Majukumu Yetu
Tunajitahidi kutoa huduma kwa uangalifu na kwa wakati unaofaa. Hata hivyo:
- Hatuhakikishii matokeo yanayotegemea mamlaka za nje (leseni, TIN, NIDA n.k.).
- Hatuhusiki na kuchelewa au kukataliwa kutokana na taarifa zisizo sahihi ulizotoa.
- Huduma zinaweza kusitishwa kwa muda kwa matengenezo au sababu za kiufundi.
7. Marejesho na Kughairi
Tazama Sera ya Marejesho na Kughairi kwa maelezo kamili.
8. Mabadiliko ya Huduma na Bei
Tunaweza kubadilisha bei, huduma, au masharti haya. Mabadiliko muhimu yataonekana kwenye app. Kuendelea kutumia huduma baada ya mabadiliko kunachukuliwa kama kukubali.
9. Sheria Zinazotawala
Masharti haya yanatawaliwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro itatatuliwa kwa amani kwanza; ikiwa haitafanikiwa, mahakama zenye mamlaka nchini Tanzania.
10. Mawasiliano
Maswali kuhusu masharti haya: Mawasiliano au chat ndani ya app.